FIZI LAZIMA IKOMBOLEWE, ASENDE MONET PELELO KUGOMBEA MMBUNGE WA TARAFA LA FIZI

kashifre

Kwajina la baba naitwa ASENDE MONET PELELO. Najulikana kwa jina maarufu KASHIFRE. Mimi ni mzaliwa wa nchi ya Jamhuri ya Kidemokratia Ya Kongo. MUBEMBE kutoka katika tarafa ya Fizi. Mimi nilikuwa mkimbizi katika kambi ya wakimbizi nchini Tanzania hapo Nyarugusu.

Katika maisha yangu nimekumbana na mambo mengi sana ambayo yamenishtua na kuamua kuchukua jukumu kama raia wa taifa ao nchi ya Kongo. Mimi nimetokea nchini Kongo ambapo ndio kwenye makao ya babu wa mababu zangu. Kabila langu ni Mubembe kutoka huko kwenye tarafa ya Fizi nchini Kongo. Ni masikitiko yangu kuona jinsi ghani ndugu zangu wanaoishi huko Fizi wanavyohangaika na kukosa mtu mbadala wa kusimamia haki yao ambayo inanyanyaswa kila kukicha. Wake zetu na watoto wetu wanawake wanabakwa, wababa zetu wana uawa, vijana wetu wanashikwa na kufungwa kwa makosa ambayo awajawahi kuyafanya. Haya ni baazi ya nusu ya mambo ambayo yananikera sana wakati huko kwetu tuna wandugu zetu katika nafasi kubwa katika serekali ambao wanashindwa kusaidia watoto wetu huko Fizi ni kitu cha kushangaza sana na kulilisha sana.

Hapa Canada mimi ni raisi ao msimamizi wa EMO YA MMBONDO. Sikuja huku Canada ili nije nikae niendelee kuvumilia jinsi ghani watoto wetu hapo Fizi wanazidi kutendewa mabaya katika maisha ya kila siku. Nilikuwa nandoto kila siku nikisema nikienda huko kwenye nchi ya tatu itabidi nijitoe kuwasaidia watoto wetu wa Fizi ikiwa kwenye wakati uho kutakuwa bado na hali ambazo sio nzuri na zenye azijatengemana.

Kwa wakati uhu naona hali imeendelea kuwa mbaya kabisa hapo Fizi na nimeamua kwenda kuwatetea ndugu zangu. Hakuna yeyote ule ambaye atatutetea ikiwa sisi wenyewe ambao tumepata bahati ya kuja huku kwenye nchi ya tatu. Nimeamua kwenda kusaidia ndugu zetu hapo Fizi na kama ujuavyo siwezi wasaidia ndugu zangu bila kuwa katika kugombea ukuu katika tarafa hilo la Fizi. Sitokubali sana ndugu zangu wazidi kuhangaika huko Fizi. Kwa njia ihi naenda moja kwa moja kugombea kwenye nafasi ya Depute ao mmbunge wa Tarafa la Fizi na nitahitaji ndugu zangu Wabembe kuwa na mimi bega kwa bega ili kuhakikisha watoto wetu wa Fizi wanakombolewa katika matatizo yanayowakumba kwa wakati uhu.

Nipo tayari kabisa katika kupoteza nguvu zangu zote katika kuhakikisha watoto wetu wa Fizi wanakombolewa katika yale matatizo ya woga walio nayo kule, mimi sitoacha kuwasaidia kwa maana ndugu zangu wanahumia sana na sisi tukikaa kimya hakuna wakuwasaidia.

Tulipo muhuliza ndugu Kashifre kuhusu yeye atagombea kwenye kiti cha chama ghani alituambia hajapenda kuongelea kuhusu chama kwa wakati uhu maana yeye anahangalia chama muhimu ni watoto wa Fizi ambao kila kukicha wanasumbuliwa na matatizo ya kila siku bila kusaidiwa na wale walio wachagua. Kwake anaona umuhimu sio kugombea kwajili ya tumbo yako binafsi unapaswa kuwa unafanaya kazi hiyo kwajili ya wanaFizi kwa ujumla.

Kwa sasa tunaweza kumuita mgombe Mbunge ASENDE MONET PELELO KASHIFRE wa Tarafa ya Fizi. ambaye ana ujumbe kwamba Fizi inapaswa kuokolewa na watoto wa Fizi wanalia YAMETOSHA.

Tutaendelea kukujuza yale ambayo yatakayo endelea kutoka kwa KASHINDI MONET PELELO KASHIFRE.