UKRISTO SIO DINI NI UHUSIANO WETU NA YESU KRISTO

Kipindi: Mjadala, Siku: Jumamosi, Mda: 13:30 – 14:30 Europe, 14:30 – 15:30 Tanzania

Mtangazaji: Emanuel Mchimbwa

Karibu tena ndugu msikilizaji wa umojaradio na msomaji wa website ihi kwenye kile kipindi cha MJADALA ambao mada yenyewe ni ” UKRISTO SIO DINI ILA UHUSIANO TULIONAO NA YESU KRISTO” ikiwa ni sehemu ya kwanza ya mahubiri yangu naomba tuwe pamoja na ukiwa makini katika roho yaKo, basi utafanikiwa vya kutosha. Ubarikiwe kwajina la Yesu Kristo unapokwenda kusoma.

Tuanze na kitabu cha Matayo 22:1: Yesu akajibu akawaambia tena kwa mitHali akisema, ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyemfanyia mwanawe arusi akawatuma watumwa wake wawaite walio alikwa, nimeaandaa karamu yangu ng’ombe zangu na vinono vimekwisha kuchinjwa, na vyote vimekuwa tayari njoni arusini. Hebu tuhangalie versi yetu ambayo tutawekea nanga kwa siku ya leo ambayo ni ile versi ya 37. Maana yake Matayo 22:37. Yesu akamwambia mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili yako yote. ihi ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. Huku ndiko tuendako sasa msomaji wangu. Baada ya hapo hebu nikupeleke kweye kitabu cha Yohana 21:15 : Basi walipomaliza kula, Yesu akwamwambia Simoni Petro, Je Simoni wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa? Akamwambia, naam Bwana wewe wajua kuwa nakupenda, akamwambia, lisha wanakondoo wangu.

Hebu turudi kwenye kichwa cha mada ya leo, Ukristo sio dini ila ni Uhusiano tulio nao na Yesu Kristo. Ndugu msomaji uhusiano unakuepo pale ambapo pana upendo. Ahina ya uhusiano ninayo hongelea una hambatana na upendo. Ukristo ni uhusiano na sio dini. Kwa hilo swali ambalo tunapaswa kujiuliza ni ikiwa sisi ni wakristo tukifuatilia yale yanayotokea katika makanisa kwa siku za leo. Unakuta kanisa hili na lile awaelewani, wengine wanashitakiana na wengine wanayo maono tofauti na ya wale. Swali linabaki ikiwa sisi ni wakristo ao sisi ni watu wa dini ?

Mkristo wa kweli sio mtu wa dini maana huyo ahongozwi na misingi ya makanisa, ao  akili zetu, maana uhu sio uhusiano ambao Mungu anasubiri uwe nao ili uhitwe mkristo. Bwana wetu Yesu Kristo alikuja ulimwenguni kufufua ule ushirika kati ya Mwanadamu na Mungu. Naomba ushikilie sana neno Ushirika. Maana pale palipo na Ushirika pana uhusiano. Na pale ambapo pana Uhusiano pia pana Upendo.

Kanisa la Mwenyezi Mungu ao kwa kingereza Ministry alianzi na uhusiano na watu. Ministry inahanza na usiano na Mwenyezi Mungu na uho uhusiano unafurika kwa watu. Maana wakati unapokuwa na uhusiano na watu unapaswa kujiuliza swali uhusiano uho unafurikia ao unatoka wapi. Kwanza uhusiano na Mungu kisha na Mwanadamu. Katika hicho kitabu cha Yohana 21: 15 chukua mda wako kusoma kuanzia versi ya kwanza hadi mwisho. Ila nataka kusoma mstari wa 15 : Basi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simoni Petro, Je Simoni wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa? akamwambia, Naam Bwana wewe wajua kwamba nakupenda , akamwambia lisha wanakondoo wangu.  Mpendwa msomaji ni kitu cha kushangaza kwamba Yesu hakumuuliza Petro, unawapenda watu ? Maana kupenda watu nikuzuri kwajili ya kanisa ao Ministry, ila kumpenda Mungu ni muhimu zaidi.

Yesu hakumuuliza Simoni Petro ikiwa alikuwa na kipawa cha uongozi, kipaji cha uongeaji, hakumuuliza ikiwa alifuata semina ya Biblia ao kusoma utumishi kwenye shule za utumishi. Hivyo vitu ni vya muhimu ila hivyo si tija ao swala kwa kuwa mkristo ao kuwa na kanisa ao Ministry iliyo katika Kristo. Msingi mzuri wa Kanisa, Ministry ao Ukristo unapatikana katika lile swali la Yesu kwa Petro ” Unanipenda ?” kwanjia nyingine unao uhusiano na Yesu Kristo ? Kwa sababu uhusiano uwezi kuwa bila ya upendo. Kujua Biblia kuanza Mwanzo hadi ufunuo, Kukariri Biblia na kujuwa sana Biblia ni muhimu ila hilo sio swala katika Ukristo. Katika kanisa za leo kuna changamoto nyingi. Kuna utumiaji wa vipaji vya  asili vya mwanadamu, masomo, uwezo , hivyo vyote ni katika ujuzi wa mwanadamu ambao mwili wetu ndo mahabara. Ila kipawa cha nguvu zisizo za kawaida kutoka kwa Mungu, roho zetu ndio mahabara.

Kitabu cha 1 wakorintho 12:7 lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa roho kwa kufaidiana. kufaidiana kuna maana kwa faida ya watu wote, versi ya nane: maana mtu mmoja apewa neno la hekima na mwengine neno la maarifa apendavyo roho yeye yule. Ninachojaribu kuonesha nikwamba kipawa cha nguvu zisizo za kawaida, ao kipawa kutoka kwa Mungu kinapewa waaminifu ili kuhudumia kwa mtu mmoja kwa mengine. Na hivi vipawa vya mwenyezi Mungu vinatenganishwa sana na vipaji vya asili vya mwanadamu.  Hacha nikupe mfano mzuri: kama nataka kuongea, kwakutumia kipawa cha asili cha mwanadamu nitaongea kwa mfano mambo ya Biblia kutokana kwamba mimi nimesoma na najua kuongea na kueleza vizuri. Hapa ni utu wangu mimi mwenyewe ambao utafanya hivyo. Nitafundisha ila utu wangu ndo utachukua usukani katika mafundisho hayo (kujua kuongea, umesoma, unajua kukariri maneno). Ihi ni tofauti sana na nguvu zinazotoka kwa Mungu kupitia roho mtakatifu. Kitabu cha Yohana 14:26 lakini huyo msaidizi, huyo roho mtakatifu, ambaye baba atampeleka kwajina langu, atawafundisha yote, nakuwakumbusha yote niliyowaambia

Kanisa za leo zimechukuliwa ao kutekwa mateka na vipaji vya asili. Kuongea kwa ujuzi katika neno la Mungu, urafiki ao uwezo wa kuhamasisha wengine kumechukua kanisa. Na ihi ndio sababu ambayo inatuma shetani anaanza kupiga ngoma katika kanisa la Mungu. Vipaji vya asili vya watu wanaojiita wakristo, uwezo wa kuongea, kuhamasisha wengine ili wasikilize, kusoma sana. Maana kama unajua kuongea vizuri, unakuta bila muongozo wa roho mtakatifu unahanza kuhubiri, unakuwa mchungaji hata kama Mungu hakukuita kuwa mchungaji, watu wa kanisani watakuona unaongea vizuri, unaeleza vizuri sana ila Mungu hajakutuma na auongozwi na roho mtakatifu. Mpendwa msikilizaji kutumia vipaji vya asili katika kazi ya Mungu bila kuongozwa na roho mtakatifu ni hatari sana. Na hizi ndio sababu makanisa mengi yameundwa, kwasababu mtu anajua kuhubiri na amesoma sana, na anajuwa kuhamasisha wengine, Mungu amekutuma ?? Na unaho uhusiano na Mwenyezi Mungu ? Kila kipaji ulicho nacho kama kwamfano unapenda kuhubiri, inabidi umuombe Mwenyezi Mungu akuruhusu kuendelea na hicho kipaji maana bila hivo utakuwa wewe umepotea na shetani atakupigia ngoma.

Kuwa mkristo kitu muhimu zaidi si kazi tunazozifanya ila uhusiano tulio nao na Yesu Kristo na mazingira yale ambayo yanayozalishwa na uho uhusiano tulio nao na Yesu Kristo. Mfano ukitaka kuwa mchungaji ao una shauku ya kumfanyia Mungu kazi ya uchungaji, aitoshi kwenda shuleni kusoma Biblia. Kusoma Biblia ni vizuri sio vibaya ila vipi kuhusu ule uhusiano tunao hongelea wa wewe na Yesu Kristo? Unampenda ao unao uhusiano naye ? Maana yale tuyafanyayo kwajili ya Mwenyezi Mungu ni tafakari tu kidogo ya ule uhusiano tulionao na mwenyezi Mungu

Usisaau kwamba Ukristo wa Kweli ao Kanisa la kweli unaanza na upendo na Mungu kisha upendo uho unafurika kwa Wanadamu. Ukinipenda unapaswa kumpenda Mungu kwanza maana ukiwa umpendi Mungu uho upendo wako unatoka wapi? Kitu muhimu katika kuwa mkristo sio kazi tuzifanyazo kwajili ya Mungu bali ushirika tulio nao na mazingira yanayotokana uhusiano uho na Kristo. Ukristo sio kwenda kanisani tu, sio kusoma Biblia mwanzo mpaka ufunuo, sio kwenda kwenye masomo ya Biblia ao sio kufuata seminari nyingi. Ukristo ni uhusiano ulio nao na Mungu. Na kwa wewe kuanza uho uhusiano, sameha wote waliokukosea kuanza maisha yako mpaka sasa, toa kila kinyongo kwenye roho yako, hacha kuwaza mabaya kwenye roho yako, kisha ungama zambi zako na baadaye muhimu sasa hanza kusoma Biblia na kutafakari kama vile Mungu alivyotuambia katika Yoshua kitabu hiki cha torati kisitoke katika kinywa chako.

Mungu akubariki ili uwe mtu mpya kwajina la Yesu Kristo. AMEN.

Kwa wakati mwengine Ubarikiwe.