Ukristo sio dini sehemu 2 : Kuamini katika roho

Mwandahaji/Presenter: Emanuel Mchimbwa

Mpendwa msikilizaji wa umojaradio na msomaji wa web ihi hebu nikukaribishe kwenye sehemu ya pili ya mahubiri yetu. Kumbuka sehemu ya kwanza ulipata kuelewa kwamba ukristo sio dini bali ni uhusiano tulio nao na Yesu Kristo. Mengi zaidi kwajilia ya mada hiyo waweza kuyasoma kwakubonyeza HAPA

Kwa siku ya leo tunaingia kwenye sehemu yetu ya pili ambayo mada yenyewe ni Kuamini katika roho yako.

Tutaaanza na kitabu cha Warumi 10:1: mbele ya kwenda kwenye verse ambayo tutaongelea kwa siku yaleo, kitabu hicho kinasema: Ndugu zangu ,nitakayo sana moyoni mwangu na dua yangu nimwombayo Mungu ni kwajili yao, ili waokolewe. Hayo maombi ni kwajili ya wana wa Israeli. Kwa maana nawashuhudia kwamba wanajuhudi kwajili ya Mungu lakini si katika maarifa. Kwa maana wakiwa hawaijui haki ya Mungu, nawakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu. Kama Mkristo kupitia roho mtu ushuhudia, mtu anaajua kwamba Yesu Kristo ni haki na Ukweli. Maana tunayo haki kwa Mungu kwajili ya Yesu Kristo.

Hebu tende kwenye versi ya neno letu la leo. Tutasoma versi ya tisa maana yake warumi 10:9: kwa sababu ukimkiri Yesu kwakinywa chako yakuwa ni Bwana na kuamini moyoni mwako yakuwa Mungu alimfufua katika wafu utaokoka. Kama nilivyosema kupitia roho Mkristo ushuhudia kuwa Yesu ni haki, ila waisraeli bado awajatangaza ao kukubali kwamba Mungu alimfufua Yesu kutoka kifo. Bado awajaamini hayo.  Kumbuka mada yetu “KUAMINI KATIKA ROHO ”

Wakati unaposoma BIblia kama tulivyowahi kukujuza ni lazima usome kwa upole na unyenyekevu na ukirudilia mara kwa mara yale ambayo umeyasoma kutoka katiba Biblia. Ukifanya hivo kumbuka roho yako itahanza moja kwa moja kutenda kufuatana na yale unayoyasoma. Tukisema kwa urahisi kutafakari kuna maanisha kuwaza. Ndugu msomaji kumbuka haya yote yanatakiwa kufuatwa ili upokee Neno la Mungu katika roho yako. Maana watu wengi awajapokea neno la Mungu katika roho zao. Swali linakuja vipi unapokea neno la Mungu.

VIPI UNAPOKEA NENO LA MUNGU KATIKA ROHO YAKO

Mpoendwa msomaji unapokea neno la Mungu katika roho yako wakati unasoma Biblia kwa upole, unyenyekevu na kwakurudilia mara kwa mara. Kusoma tunakohongelea hapa sio kusoma ambako unasoma buku za shule, unajuwa wakati unasoma kwajili ya shule unasoma kwa haraka ili uelewe vile unavyovisoma. Hapa atuongelehi huko kuelewa ambako unazani ndugu yangu. Kwa neno la Mungu unapaswa kuongozwa na roho mtakatifu wakati unasoma Biblia. Na ihi ndio sababu unapaswa kusubiri roho mtakatifu akuongeze katika kusoma neno la Mungu. Unaposoma Biblia kwa upole ao unyenyekevu unayapa maneno yale mawazo yako yote. Maana ukiwa na mawazo mengi ambayo bado unayo katika roho ao unayoyawaza kwa mda uho uwezi soma kwa upole na unyenyekevu. Vile katika kusoma Biblia tunaombwa kuwa makini na yale ambayo tunayasoma. Hapa namaanisha kuwekea maanani yale ambayo unayasoma. Kwa lugha ya juu tunaweza kusema nikufunga mlango wa nje na kufungua ule wandani. Mlango wa nje mfano, kufunga contact yote ile ambayo inayoweza kukusumbua katika kusoma neno hili. Unafunga simu, unatafuta nafasi tulivu, alafu unafungua roho yako kwa kusoma kwa upole na unyenyekevu ukirudilia mara kwa mara. Maana ndugu msikilizaji kumbuka kusoma Biblia nikuongea na Mungu. Maana Mungu afanyi lolote bila kutumia neno lake, sasa sijui kwanini unachukulia kusoma Biblia kama kitu ambacho unaweza kufanya mahali pote hata sokoni. Kumbuka hilo aliwezekani maana Mungu awezi changia roho yako na kitui kingine chote.

Ndugu msikilizaji katika kusoma Biblia hiyo unaendelea kuongeza imani lako na kuona yale ambayo Mwenye Mungu anaweza kufanya katika maisha yako. Hebu niwaambie tu wkamba Imani aliwezi kuhigwa hata siku moja. Unakuta sababu mtu anaingia kanisani moja kwa moja anapiga magoti kila siku ya jumapili alafu anakaa chini sasa nawewe ukiona hayo, Mungu hata siku moja hajawahi kukuambia wkamba uwe nafuatilia hayo, ilawewe unayafanya hayo. Hiyo sio Imani, ao kwa sababu mwenzako kafunga siku kumi kasaidiwa na wewe unataka kufunga siku kumi ili nawewe usaidiwi, hapo hakuna imani. Unakuta wachungaji wanakuambia inabidi ufunge siku 21 ndo Mungu atakusikia bila hivo aiwezekani, hayo yameandikwa wapi ao kuna wachungaji wengine ambao watakuambia itabidi uombe masaa matatu ao saa kadhaa ili Mungu akusikie, hayo yote si ya kweli. Roho wa Bwana anaweza kukuweka nyumbani hata siku nzima ili uombe., roho wa Mungu anaweza kukutoa ukiwa nakula anasema hacha kula nena kaombe. Ndugu msikilizaji hili linapaswa wewe msomaji ujuwe kwamba njia za Mungu anazohongoza watu wake na kufanya kazi, hakuna anayezijua kusema ukweli. Uwe mwinjilisti, uwe mchungaji hacha roho wa Bwana akuongoze, na jinsi ghani utaongozwa na roho wa Bwana ni katika kusoma neno lake, kuhishi neno lake na kutenda neno lake.  Hayo yote yanakuja kukupeleka kwenye neno letu la leo Kuamini katika roho. Maana yale uyaaminio katika roho yanatokana na yale unayoyasoma.

Ndugu msomaji naomba tuachane na mambo ambayo tunayaita sheria za kanisa, na tuache roo mtakatifu atuingile ili roho zetu ziwe na imani tupewayo kutoka kwa Mungu. Maana asikudanganye mtu kwamba akufundishe kuongea kw alugha ya mbinguni ili akuombee kwamba uongee kwa lugha ya mbinguni apana. Imani lako litakuja katika kusikiliza neno la Mungu na kulisoma kwa upole, kwa unyenyekevu ukirudilia mara kwa mara. Soma neno sio tu kwajili ufundishe, bali uhishi na kutenda neno.
Maombi: Fungua roho yako na useme pamoja nami, Bwana Yesu Chukua yangu yote na unipe yako yote, maana mimi bila wewe siwezi lolote. Kwajina la Yesu. Amen.