About Us

Ukipenda kusoma mengi kwajili yetu, upo kwenye nafasi kamili. Soma ili ufahamu jinsi ghani Mungu alivyotuwezesha kufika pale tulipo kwa sasa.

Chairman: Imani Mchimbwa

Chairman: Emanuel Mchimbwa

Treasurer: B.F. Mchimbwa

Secretary: Emanuel Mchimbwa

Our story

Sisi ni vijana watatu ambao ni wanafamilia kwamajina Imani Mchimbwa, Byaunda Furahisha Mchimbwa na Emanuel Mchimbwa. Sisi ni wazaliwa wa nchi ya Kongo ambapo hapo awali ilihitwa Zaire. Baada ya kutokea kwa vita miaka ya 1996 kama familia tulikimbia kutoka nchini kwetu huko Kongo na kukimbia vita ambavyo viliuwa mamilioni ya ndugu zetu wakati uho. Kukimbia vita vyetu ni kitu ambacho hakuna aliyetegemea. Kutokana na hayo tumehacha kila kitu na kukimbia mikono mitupu kwa sababu maisha yetu yalipaswa kuwa na usalama mbele ya vitu tulivyokuwa navyo. Baada ya kukimbia kutoka nyumbani kwetu tulijikuta tunaelekea Tanzania ambako tulipokelewa na watu wa UNHCR huko tanzania na kuwekwa katika kambi ya wakimbizi ya Tanzania kwajina la Nyarugusu. Katika kambi hiyo tulihishi karibia miaka kumi na moja (11).

Katika kambi ya wakimbizi tuliendelea na maisha yetu ya kawaida ambayo ni kila siku kumtegemea Mungu na kuendelea kusikiliza neno lake. Baada ya mda mwaka wa 2007 Mungu katujalia na tukachaguliwa kwenda Ulaya ili kwenda kuendeleza maisha yetu huko. Hiyo ndo sababu ya sisi kuja hapa Uholanzi ambako tunaishi zaidi ya miaka 10. Tujuwe kwamba njia ya kufika hapa tulipo ahikuwa njia rahisi na ndio maana kila siku uwa tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutufikisha hapa tulipo. Wengi walitaka wafike ila awakupata nafasi ya kufanikisha hayo. Ila sisi Mungu ni mkuu ametuchagua na kutupa na fasi ihi. Baada ya kufika hapa Uholanzi tulitaka kuendeleza kutangaza Neno la huyo Mungu wetu aliye tuleta hapa Ulaya. Mwaka wa 2014 tukafungua kampuni yetu kwajina la Stichting Umoja Radio ambayo inasajiliwa kwa namba za K.V.K. 61024007.